Siku ya Matendo Mema ilianzishwa mwaka 2007 na mfanyabiashara na mhisani mwanamke, Shari Arison, Aidha, ilizinduliwa na kuandaliwa na Ruach Tova (Asasi Isiyo ya Serikali – AISE), sehemu ya Mfuko wa Familia ya Ted Arison, Tawi la Kampuni ya Arison. “Ninaamini kwamba kama watu watafikiria mambo mema, kuzungumza mema na kutenda mema, mzunguko wa kutenda wema utaongezeka duniani. Siku ya Matendo Mema imekuwa siku yenye mwamko mkubwa wa utoaji wa matumaini, na mwaka huu watu binafsi, watoto wa shule, wanajeshi na wafanyakazi kutoka katika shughuli nyingi mbalimbali wanaungana kwa ajili ya Siku ya Matendo Mema ya mwaka kwa lengo la kufanya matendo mema kwa wengine, “ anasema Shari Arison.
Siku ya Matendo Mema inaenea duniani kote!
Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2007, mazoea haya ya kila mwaka ya mambo mema yameongezeka kutoka washiriki 7,000 mwaka 2007 huko Israel hadi washiriki wapatao milioni 1 mwaka 2015. Ilisambaa duniani kote mwaka 2011 katika miji ya kimataifa 10, mingi ikiwa ni kutoka Marekani, Siku ya Matendo Mema ilianza kwa kuwaunganisha watu duniani kote. Mwaka 2012, tulifika Ulaya na kushirikiana na MTV Global katika kampeni ya wiki sita kwenye mtandao wake na majukwaa ya Televisheni tukionyesha ujumbe kwa watazamaji milioni 24 duniani kote. Mwaka 2013, watu wa kujitolea 16,000 kutoka nchi 50 walishiriki katika mamia ya miradi, ikiwemo ule ulioanza ambao ulifanywa na Mtandao wa ABC katika Jiji la New York. Baada ya hapo, Siku ya Matendo Mema iliongezeka mara mbili katika kuwafikia watu mwaka 2014, kwa kushirikiana kwa mwaka wa pili mfululizo na Mtandao wa ABC wa Jiji la New York, na kwa kushirikiana na mashirika makubwa ya kujitolea kama sehemu ya kampeni kubwa inayohusisha Televisheni, redio, na mitandao ya kijamii. Watu 500,000 walishiriki huko Israel na watu wapatao 35,000 duniani kote.
Siku ya Matendo Mema iliendelea kupata kasi na kufanya siku yake kuu kuwa tarehe 7 Aprili, 2019. Washiriki 3,900,000 kutoka katika nchi 108 walishiriki katika miradi 20,000, yenye jumla ya zaidi ya saa milioni 7.8 za kutoa huduma.
Miradi ya Siku ya Matendo Mema inafanyika duniani kote kupitia washirika wenyeji na wawakilishi.
Baruapepe: info@good-deeds-day.org